Real Madrid imeendelea kuonyesha nguvu zake kwenye Laliga, baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Deportivo Alavés katika mechi iliyofanyika leo. Huu ni ushindi muhimu ambao unasaidia Real Madrid kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, ikiwa alama nne nyuma ya vinara Barcelona.
Kylian Mbappé amefunga bao lake la 17 msimu huu katika mechi yake ya 17 ya ligi, akithibitisha kuwa bado ni miongoni mwa washambuliaji bora wa dunia. Bao la kwanza la mechi lilifungwa na Mbappé dakika ya 24, likifungua njia ya ushindi wa Los Blancos.
Bao la ushindi la Real Madrid lilifungwa na Rodrygo, akimalizia dakika ya 76, baada ya Alavés kuwa tayari wamepata bao la kufutia machozi kupitia Vicente dakika ya 68.
Tokeo la Mwisho (FT):
Alavés 1-2 Real Madrid
24’ Mbappé
68’ Vicente
76’ Rodrygo
Ushindi huu unaendelea kuonyesha umuhimu wa Mbappé na Rodrygo kwenye safu ya mbele ya Real Madrid, huku timu ikijaribu kupunguza pengo la alama nyuma ya Barcelona vinara wa ligi.






