Vin Diesel amethibitisha hadharani kwamba staa wa soka Cristiano Ronaldo anaweza kushiriki katika filamu ijayo ya Fast & Furious, ambayo huenda ikawa ni sehemu ya mwisho, Fast X: Part 2.
Kupitia chapisho la Instagram lenye picha ya wawili hao wakiwa pamoja, Diesel aliandika: “Kila mtu aliuliza, angekuwa katika simulizi za Fast … I gotta tell you he is a real one. Tuliandika jukumu kwa ajili yake … “.
Ronaldo anatazamiwa kucheza filamu ya mwisho ya Fast & Furious, ambayo mara nyingi hujulikana kama Fast & Furious 11 au Fast X: Sehemu ya 2, ambayo ina tarehe ya kuachiwa mnamo Aprili 2027.
Ingawa maoni ya Diesel yanaashiria nia ya dhati, wafuasi wa fimamu hiyo wanasubiri uthibitisho rasmi kutoka kwa nyota huyo wa kandanda mwenyewe.






