
TETESI: Beki wa kulia wa kimataifa wa Afrika Kusini, Khuliso Johnson Mudau (Mamelodi Sundowns), anatajwa kuwa karibu kujiunga na Young Africans SC (Yanga) mwezi Januari!
Vigogo wa Yanga wanaripotiwa kumpa Mudau ofa nono ili asiongeze mkataba na Sundowns, ikiwemo:
🔹Dau la Kusajili (Signing Fee): TZS 900 MILIONI
🔹Mshahara: TZS 40 MILIONI kwa Mwezi
(NB: Mkataba wa Mudau na Sundowns unamalizika hivi karibuni)
📊Kama usajili huu wa Mudau utafanikiwa, utaibua maswali makubwa katika kikosi cha Yanga, hasa upande wa beki wa kulia:
🔹Kouassi Attohoula Yao: Amerejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu (karibia msimu mzima) kutokana na majeraha. Uwezo wake wa kutoa asisti na kupanda mashambulizi unajulikana. Je, ujio wa Mudau utampunguzia nafasi?
🔹Israel Mwenda: Amekuwa kipenzi cha mashabiki na amekuwa bora katika kuziba pengo la Yao. Amecheza kwa kiwango cha juu sana. Je, anapoteza nafasi yake ya kwanza na sasa anakuwa chaguo la 3?
🔹 Kibwana Shomari Je?
Je, unaona Yanga wataweka ubora wa kikosi mbele (Mudau) au watazingatia ukweli kwamba tayari wana mabeki wawili bora (Yao na Mwenda)? 🤔
The post Yanga Hii Sasa SIFA, Wanaenda Kuibomoa Mamelody Kwa Kumchukua Beki Huyu appeared first on SOKA TANZANIA.





