
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kitai – Luanda wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, Desemba 16, 2025. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kumsimamia mkandarasi anayejenga barabara ya Kitai hadi Ruanda ili akamilishe ujenzi wa barabara hiyo muhimu kwa wakazi wa mkoa huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).






