Singida Black Stars imeelekeza nguvu zake kwa beki wa kimataifa wa DR Congo, Henock Inonga, kama chaguo la kwanza kwa ajili ya kuimarisha ukuta wa kikosi hicho dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa Januari Mosi 2026 kutokana na mapendekezo ya Kocha Miguel Gamondi.
.
Taarifa kutoka katika klabu hiyo, zinaeleza Gamondi amekuwa akihitaji beki wa kati mwenye uzoefu mkubwa na uwezo wa kuhimili presha ya mechi kubwa, jambo linalomfanya Inonga kuibuka kama jina linalopewa uzito zaidi kuliko machaguo mengine yaliyopo
.
Inonga, ambaye kwa sasa hana timu baada ya kumaliza mkataba wake na FAR Rabat ya Morocco, inaelezwa yupo tayari kurejea Ligi Kuu Bara, hatua inayoipa Singida fursa ya kumsajili.
.
Uamuzi wa Singida kumtazama Inonga kwa karibu umechochewa pia na changamoto za kiufundi zinazoikabili timu hiyo na Gamondi amelazimika kumrudisha kiungo Morice Chukwu kucheza nafasi ya beki wa kati akishirikiana na Antony Tra Bi, hali inayoonesha wazi kocha huyo bado hajaridhishwa na kiwango cha mabeki wa asili waliopo kikosini
The post Singida Black Stars Wanamtaka Beki HENOCK Inonga Kwa Udi na Uvumba appeared first on SOKA TANZANIA.





