Kampuni ya Meridiansport imeendelea kuonesha dhamira yake ya kijamii kwa kuwatembelea watoto yatima wa Faraja Care Orphanage Centre Mburahati, ikiwaletea furaha na matumaini mapya. Ziara hiyo ililenga kuonyesha mshikamano na upendo kwa watoto hao, huku ikichangia moja kwa moja katika ustawi wao wa kila siku na katika maandalizi yao ya kielimu.
Wakati wa ziara hiyo, Meridiansport iliwakabidhi watoto vifaa muhimu vya shule kama mabegi, madaftari, vitabu na kalamu, zawadi za msimu wa sikukuu. Msaada huu ulilenga kuwapa watoto hao nguvu na motisha ya kuendelea na masomo yao bila hofu ya kukosa vifaa vya msingi, huku ukiwa ni maandalizi muhimu kuelekea kuanza kwa mwaka mpya wa masomo Januari hii.
Nancy Ingram, mwakilishi wa Meridiansport, alisisitiza kuwa kampuni hiyo haifanyi biashara peke yake, bali pia ina wajibu wa kijamii. “Watoto wetu wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo huwapunguza motisha ya masomo. Ni jukumu letu kuwasaidia kwa vitendo, kuhakikisha kila mtoto anahisi upendo, usalama na kuthaminiwa,” alisema.
Meridiansport inakupa taarifa mbalimbali za michezo ya kitaifa & kimataifa pamoja na uchambuzi wa michezo mbalimbali. Ingia leo kupitia meridiansport.co.tz na uanze kuburudika kwa taarifa mbalimbali za hapo kwa hapo ndani na nje ya nchi.
Watoto na walezi wao walipokea msaada huo kwa furaha kubwa na shukrani, wakieleza kuwa zawadi hizo zitawasaidia kushughulikia changamoto za kila siku na kuwa na motisha ya kuendelea na masomo bila vikwazo. Msaada huu umeongeza imani na matumaini kwa watoto hao kuwa jamii bado inawathamini na kuwajali.
Hii ni sehemu ya mpango mpana wa Meridiansport wa uwajibikaji wa kijamii, unaolenga kusaidia sekta za elimu, afya na mazingira. Sambamba na jitihada hizi, Meridiansport inawapa wasomaji wake uhakika wa habari za michezo zilizoandaliwa kwa kina.
The post WATOTO YATIMA WAPATA FARAJA NA MERIDIANBET appeared first on Soka La Bongo.





