

Askofu Mkuu wa Kanisa katoliki Jimbo la Dar Es Salaam, Jude Thaddeus Ruwa’ichi amesema katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo(Christmas) ni vyema Watanzania wakachukua somo la kutenda haki ambalo ni sifa katika miongoni mwa sifa za Yesu.
Ameyasema hayo wakati wa Misa ya Mtakatifu Mkesha Noeli 2025 iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jimbo Kuu la Dar Es Salaam usiku wa Disemba 24, 2025.
“Naomba nithubutu kusema kwamba Watanzania wengi hawashabikii haki, sio wadau wa haki, Watanzania wengi kwa ujinga, kwa kurubuniwa au kwa vinginevyo ni au wanajidai kuwa wadau wa amani”
Ameeleza kuwa ili kuwa na amani ya kweli ni vyema haki ikazingatiwa kwanza.
“kama unataka kujigamba kuwa mtu wa amani, jitose kupigania haki, jitose kusimamia ukweli” amesema Ruwa’ichi
The post Askofu Ruwa’ichi Acharuka ‘Waliomshitaki Padre Kitima Ni Wasaliti’ — VIDEO” appeared first on Global Publishers.







