

Kikosi cha Timu ya soka ya Taifa Taifa Stars kinachoshiriki Michuano ya AFCON 2025 huko Morocco, kimefanya Mazoezi kuelekea mechi yake ijayo kesho Desemba 27 dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’
Stars itakutana na Ndege hao wa Uganda maarufu kama ‘Korongo Mwenye Tai’ (The Cranes), katika mechi muhimu ambayo inapaswa kushinda ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele katika Michuano hiyo baada ya kuanza vibaya kwa kichapo cha Mabao 2-1 toka kwa Nigeria juzi.
The Cranes nao hawajaanza vizuri Michuano hiyo baada ya kuanza na kipigo cha mabao 3-1 toka kwa Tunisia.
Mazoezi ya Taifa Stars leo yamefanyika kwenye Uwanja wa Academic Mohammed VI, Rabat, Morocco.

The post Taifa Stars Yajiandaa Kuikabili Uganda ‘The Cranes’ Michuano ya AFCON 2025 appeared first on Global Publishers.







