Klabu ya Singida Black Stars itacheza mchezo rasmi wa ufunguzi wa michuano ya Mapinduzi Cup dhidi ya Mlandege siku ya leo katika dimba la New Amaan majira ya saa 10:15 jioni.
Singida Black Stars tayari imewasili visiwani Zanzibar siku ya jana na kufanya mazoezi ya kurejesha utimamu wa miili ya wachezaji ili kujiweka sawa kuelekea mtanange huo.
“Singida Black Stars tumepata heshima kubwa kucheza mechi ya kwanza ya uzinduzi wa Kombe la Mapinduzi 2026” Amesema Meneja Habari na Mawasiliano wa timu hiyo – @massanzajr




