KLABU ya Simba imemtangaza rasmi Sibusiso Makhula kuwa kocha mpya wa viungo wa kikosi cha timu hiyo, hatua inayolenga kuimarisha zaidi maandalizi ya wachezaji kimwili kuelekea mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa.
Makhula, ambaye ni raia wa Afrika Kusini, anajiunga na Simba akiwa na uzoefu wa kutosha katika masuala ya mazoezi ya viungo na maandalizi ya wachezaji kwa viwango vya juu vya ushindani.
Mbali na kufanya kazi katika klabu mbalimbali ikiwemo Sekhukhune United, kocha huyo amewahi pia kuhudumu katika benchi la ufundi la timu ya taifa ya Afrika Kusini, jambo linaloonyesha kiwango na ubora wa taaluma yake katika sekta ya soka.
Uongozi wa Simba umeeleza kuwa ujio wa Makhula ni sehemu ya mkakati mpana wa kuimarisha benchi la ufundi, hususan katika eneo la maandalizi ya viungo ili kuongeza nguvu, kasi na uimara wa wachezaji ndani ya uwanja.
Kwa upande wake, Makhula ameonesha furaha kubwa kujiunga na klabu ya Simba, akiahidi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana kwa karibu na benchi la ufundi pamoja na wachezaji ili kufikia malengo ya klabu.
The post KOCHA WA VIUNGO ATAMBULISHWA MSIMBAZI appeared first on Soka La Bongo.






