KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi mpango wa usajili wa klabu hiyo katika dirisha dogo la mwezi Januari, amesisitiza kuwa timu yake inahitaji kuongeza nguvu katika maeneo kadhaa muhimu.
Imeelezwa kutoka ndani ya klabu hiyo kuw Barker amesema lengo ni kuboresha ushindani wa kikosi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupambana kwenye mashindano ya ndani na ya kimataifa.
Mtoa habari huyo amesema kocha amewaleza kuwa Simba inahitaji kusajili mchezaji wa nafasi ya beki wa kushoto (left-back), kiungo namba , kiungo namba pamoja na winga wa kulia.
“Barker ameeleza kuwa nafasi hizo zimeonekana kuwa na uhitaji mkubwa kutokana na ratiba ngumu na mahitaji ya mbinu za kisasa anazotaka kuzitumia kikosini,” amesema mtoa habari huyo.
Amessma klabu inatafuta beki mmoja wa kati ili kuongeza uimara wa safu ya ulinzi, anapaswa kuwa na uzoefu, uwezo wa kusoma mchezo na kuongoza wachezaji wenzake, hasa katika mechi zenye presha kubwa.
“Simba itaangalia pia vipaji vya ndani, lakini kwa baadhi ya nafasi maalum, macho yameelekezwa zaidi nje ya Tanzania ili kupata ubora unaohitajika kwa haraka,” amesema.
Mtoa habari huyo ameongeza kuwa wachezaji wawili wa kigeni waliopo kwenye rada ya klabu hiyo wanatoka Afrika Kusini, ambapo mmoja ni kiungo namba na mwingine ni winga.
Amesema Barker anawafahamu vizuri wachezaji hao na anaamini wanaweza kuleta mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Simba na uongozi wa Simba SC unaendelea na mazungumzo pamoja na tathmini ya kina kabla ya kukamilisha usajili huo.
Mashabiki wa klabu hiyo wanaendelea kusubiri kwa hamu kuona majina ya wachezaji watakaovaa jezi nyekundu na nyeupe, huku matarajio yakiwa ni kuona timu ikirejea katika ubora wake wa ushindani.
The post SIMBA NAFASI TANO KUIMARISHA KIKOSI appeared first on Soka La Bongo.





