DAR ES SALAAM;SANURA Kasimu maarufu kama Mama Dangote amethibitisha kuwa alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kushiriki moja kwa moja katika harakati za matibabu ya Mkubwa Fella, akisisitiza umuhimu wa kuthamini na kushukuru msaada unaotolewa na watu mbalimbali katika nyakati za shida.
Kupitia ujumbe aliouchapisha, Mama Dangote amekumbusha jamii kuhusu thamani ya shukrani pale mtu anapojitoa kusaidia mwenzake, akisema kuwa msaada wa dhati haupaswi kubezwa.
“Binadamu tushukuru. Mtoto wa mtu akijitoa kwenye jambo la mtu, tuwe na shukrani,” ameandika Mama Dangote.
Katika hatua nyingine, Esma Platnumz ambaye ni dada wa msanii Diamond Platnumz, amechapisha ujumbe wa kumtia moyo mdogo wake kupitia ukurasa wake wa Instagram, huku akisisitiza kuwa kusaidia wengine ni jambo lenye baraka kubwa na halipaswi kukatisha tamaa.
Esma amebainisha kuwa msaada unaotolewa kwa nia njema hulipwa na Mwenyezi Mungu, akiwahimiza watu kuendeleza moyo wa kujitoa bila kuvunjika moyo.
“Mungu atakulipia mdogo wangu Inshallah. Usikate tamaa wala kuvunjika moyo kusaidia wengine.
Binadamu tushukuru mtoto wa mtu akijitoa kwenye jambo la mtu,” ameandika Esma Platnumz.
The post Mama Dangote, Esma Platnumz wasisitiza shukrani katika msaada wa Mkubwa Fella first appeared on SpotiLEO.





