RABAT:SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemuondoa mwamuzi wa kimataifa wa Mali, Boubou Traoré, katika orodha ya watakaosalia kuchezesha mechi zilizobaki za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazoendelea nchini Morocco.
Mbali na Traoré, mwamuzi mwingine aliyeripotiwa kuondolewa ni Abdou Abdel Medire kutoka Cameroon aliyechezesha mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Nigeria dhidi ya Msumbiji.
Traoré ndiye aliyechezesha mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Taifa Stars na Morocco, mchezo uliogubikwa na maamuzi yaliyotajwa kuwa ya utata na kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka barani Afrika
Inaelezwa kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mchakato unaoendeshwa na CAF wa kufanya tathmini ya viwango na utendaji wa waamuzi waliokuwa wakisimamia michezo ya AFCON, lengo ni kuona haki na ubora wa maamuzi katika hatua nyeti za mashindano.
The post Mwamuzi wa Stars mechi ya Morocco aondolewa first appeared on SpotiLEO.





