MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC, Libasse Gueye, ametoa wito mzito kwa mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuisapoti timu yao kwenye mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esperance Sportive de Tunis.
Simba itashuka dimbani Jumapili, Februari Mosi, katika mchezo wa marudiano dhidi ya Esperance, ikisaka ushindi na alama tatu zitakazoipa nguvu kubwa katika mbio za kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Mchezo huo unatajwa kuwa wa presha kubwa, huku kila pointi ikiwa na thamani muhimu kwa hatma ya timu hizo kwenye kundi.
Gueye ameendelea kujipatia heshima kubwa kwa mashabiki wa Simba baada ya kung’ara katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa FC.
Ambapo aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo na kuifungia Simba bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0. Uchezaji wake umeongeza matumaini mapya ndani ya kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.
Mshambuliaji huyo amesema anajivunia kuanza vyema safari yake akiwa na Simba, akisisitiza kuwa ushindi huo wa ligi ni motisha muhimu kuelekea pambano gumu la Jumapili dhidi ya Esperance.
Gueye ameongeza Ameeleza kuwa anajisikia tayari kuendelea kutoa mchango wake kwa timu katika michezo ijayo kuwa morali ndani ya kikosi ipo juu, huku maandalizi yakiendelea vizuri chini ya benchi la ufundi.
Ameongeza kuwa lengo likiwa ni kuhakikisha Simba inaingia uwanjani ikiwa tayari kupambana kwa dakika zote 90 kutafuta matokeo chanya mbele ya wapinzani wao kutoka Tunisia.
“Wanasimba wote wajitokeze kwa wingi Jumapili kuisapoti timu yao. Hautakuwa mchezo rahisi, lakini tutaingia kupambana kwa ajili ya klabu na kuhakikisha tunapigania ushindi,” amesema Gueye,
The post GUEYE ACHOCHEA VITA DHIDI YA ESPERANCE appeared first on Soka La Bongo.





