KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, amefunguka kuhusu mshambuliaji wao Laurindo Dilson Maria Aurélio maarufu kama Depu, akisema licha ya kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani bado ana mengi ya kujifunza ili kufikia kiwango chake cha juu.
Pedro amesema Depu ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, lakini bado anakumbana na changamoto ndogo ndogo za kiufundi na kimbinu zinazomzuia kuonyesha uwezo wake wote kwa ukamilifu ndani ya uwanja.
Kocha huyo raia wa Ureno ameeleza kuwa jukumu la benchi la ufundi ni kufanya kazi kwa karibu na mshambuliaji huyo ili kumsaidia kuboresha maeneo anayohitaji marekebisho na hatimaye kufikia ubora anaoutamani.
“Depu ana nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kufunga mabao, lakini bado anahitaji utulivu zaidi anapopata nafasi za wazi ili kuzitumia kwa manufaa ya timu,” amesema Pedro.
Ameongeza kuwa Depu ni miongoni mwa wachezaji wanaojituma kwa kiwango kikubwa mazoezini na ana kiu ya mafanikio, hali inayompa matumaini makubwa kuwa atakuwa silaha muhimu kwa Yanga katika michezo ijayo.
Pedro pia amewaomba mashabiki wa Yanga kuwa wavumilivu kwa mshambuliaji huyo, akisisitiza kuwa maendeleo ya mchezaji ni mchakato unaohitaji muda, imani na sapoti kutoka kwa kila mmoja ndani na nje ya uwanja
The post DEPU BADO ANA SAFARI NDEFU, PEDRO appeared first on Soka La Bongo.





