DAR ES SALAAM: Mwanamitandao maarufu, Clemence Mwandambo, amewapa somo vijana kuhusu masuala ya mahusiano, akisisitiza kuwa si busara kurudiana na mpenzi wa zamani (Ex).
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Mwandambo amedai kuwa mwanamke hapendi kuachwa mara mbili, hivyo endapo mwanaume atarudiana na mpenzi wake wa zamani, anaweza kukumbana na changamoto au madhara makubwa baadaye.
“Ex harudiwi. Mwanamke hapendi kuachwa mara mbili, hivyo akirudi kwako anaweza kukufanyia jambo lolote ili kuhakikisha haumwachi tena. Unaweza kujikuta ukijuta,” amesema Mwandambo.
Katika kauli yake, aligusia pia sakata la wasanii Harmonize na Kajala, akieleza kuwa kurudiana kwao ni jambo lisilo na busara kwa upande wa Harmonize, japokuwa amesisitiza kuwa hakumaanishi Kajala anaweza kufanya vitendo hivyo alivyovitaja.
Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa mitandaoni, ambapo baadhi ya watu wameunga mkono ushauri huo huku wengine wakipinga wakisema mahusiano hutofautiana kulingana na watu husika.
Maoni yangu
Kauli ya Clemence ina ujumbe wa tahadhari, lakini imejaa ujumla (generalization).
Si kila mahusiano ya “Ex” ni mabaya wala si kila mwanamke au mwanaume huumiza akirudiwa.
Kuna watu hurudiana, wakarekebisha makosa, na kuishi vizuri kabisa.
Hata hivyo, funzo kubwa hapa ni kujitathmini:
The post Mwandambo atoa onyo kwa vijana kurudiana na “Ex” first appeared on SpotiLEO.






