ZANZIBAR: TAMASHA la Sauti za Busara linalofanyika mwezi Februari kila mwaka kwa mwaka 2027 litafanyika mwezi Machi ili kupisha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani utakaofanyika ndani ya mwezi wa Februari.
Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Journey Ramadhani ametaja tarehe ya Tamasha hilo kwa mwakani kuwa ni Machi 11 hadi 14.
“Tamasha huwa likifanyika kila mwezi wa pili kila mwaka lakini kwa mwakani tumebadilisha kidogo ambapo badala yake litafanyika mwezi wa tatu baada tu ya mfungo wa Ramadhani utakaofanyika mwezi wa pili lakini pia Tamasha letu litafanyika kwa mara ya pili hapa hapa Viwanja vya Mnazi Mmoja” amesema Journey Ramadhani.

Ramadhani amesema watapeleka mapendekezo mapema kwa Serikali ya Zanzibar ili waendelee kuwapa eneo la Mnazi Mmoja liwe na muendelezo wa Tamasha hilo hata kama jengo la Ngome Kongwe litakamilika kwa maboresho.
“Tutaiomba Serikai ya Zanzibar itupe tena eneo hilo la Mnazi Mmoja ili tufanye tamasha letu kwa mwakani maana hapa tuna nafasi kubwa ya kufanya tamasha tutakavyo na kulingana nae neo lilivyo tofauti na Ngome Kongwe ilikuwa tunalazimishwa na udogo wa eneo,” amesema Ramadhani.
The post Tamasha la Sauti za Busara 2027 kupisha Mfungo first appeared on SpotiLEO.




