SERIKALI imepiga marufuku matumizi ya mitandao binafsi zikiwemo baruapepe, WhatsApp, Instagram, You Tube, Facebook kutuma nyaraka na taarifa za serikali. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ametangaza amri hiyo wakati akifunga kikaokazi cha sita cha Serikali Mtandao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) jijini Arusha





