Shirika la Afya Duniani (WHO) na lile la Marekani CDC yametangaza kuwa, kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa surua kiliongezeka duniani kwa asilimia 20 kati ya mwaka 2022 na 2023.
Takribani watu 110,000 walikufa wengi wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Ripoti ya mashirika hayo inaeleza kuwa, milipuko mikubwa zaidi ilitokea katika nchi ambazo watoto walikuwa na lishe bora na wangeweza kustahimili ugonjwa huo na ambako kulikuwa na huduma bora za afya.
Mamlaka hizo za afya duniani zimesema kuwa, surua moja ya magonjwa ya kuambukiza duniani ni ugonjwa ambao unaweza kuzuilika kupitia dozi mbili za chanjo.
Duniani kote asilimia 83 ya watoto hupatiwa chanjo ya kwanza lakini ni asilimia 74 wanaopokea chanjo ya pili. Jumla ya nchi 57 ziliripoti milipuko ya surua mwaka 2023, karibu nusu zikiwa za Afrika.
Wataalamu wa afya wanasema, ugonjwa wa surua unasababishwa na virusi na unaweza kumpata mtu wa rika lolote ila huathiri zaidi watoto. Dalili za awali za surua ni koo kuuma, kikohozi, homa na madoa ya rangi ya kijivu au nyeupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu
The post Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa surua chaongezeka :WHO first appeared on Millard Ayo.