Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini India.
Taarifa
iliyotolewa na Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) imeeleza kuwa
kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile
kimechotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India
alipokuwa akipatiwa matibabu.

“Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na
Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika,
Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulle. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa
familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze
roho ya marehemu mahala pema peponi”, amesema Spika.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.