Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs
Mwambegele, akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na
Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Arusha ikiwa
ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao
unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na
Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za
Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa
Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya
Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa
Rufaa(Mstafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mkutano
wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29,
2024 mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024.
Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini,
Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi
wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa
Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa
Kimila.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa
Rufaa(Mstafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mkutano
wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29,
2024 mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs
Mwambegele, akizungumza wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau
wa Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 29, 2024 mkoani Arusha ikiwa ni
maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao
unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao ni pamoja na
Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za
Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa
Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya
Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila. Kulia ni
Mkurugenzi wa Uchagizi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima
Ramadhani.
Mjumbe wa Tume Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akifuatilia mada wakati wa mkutano.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw. Kailima
Ramadhani akiwasilisha mada ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga
Kura katika mkutano huo. Mkurugenzi
wa Daftari na TEHAMA wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC),
Bw.Stansalaus Mwita akiwasilisha mada ya Mfumo wa Uboreshaji wa Daftari
katika mkutano huo. Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Daftari na TEHAMA (Daftari), Bw. Martin Mnyenyelwa
akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa wadau kuhusu mfumo wa uboreshaji
kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi
Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi Giveness Aswile akizungumza kwa niaba
ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, wakati wa mafunzo kwa wadau kuhusu
mfumo wa uboreshaji kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro. Mkurugenzi
wa Kitengo cha Huduma za kisheria wa INEC, Bw. Selemani Mtibora
akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau mkoani Kilimanjaro.
Wadau wa uchaguzi kutoka Mkoani Kilimanjaro wakiwa mkutano wa wadau.Wadau
wa uchaguzi kutoka Mkoani Arusha wakishiriki mkutano wa Tumen a Wadau
wa Uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura ambao unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17, 2024. Wadau hao
ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi
wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari,
Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi
mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Na. Mwandishi Wetu
Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Arusha na Kilimanjaro
utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024.
Akifungua
mkutano wa wadau wa uchaguzi mkaoni Arusha leo tarehe 29 Novemba, 2024,
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa,
Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji huo pia utajumuisha Mkoa wa Dodoma
kwenye Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Chemba na Mji wa Kondoa ambapo
vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa
12:00 jioni.
Amesema
mikoa hiyo inafanya uboreshaji wa Daftari ikiwa ni mwendelezo wa zoezi
hilo ambalo lilizinduliwa tarehe 20 Julai, 2024 mkaoni Kigoma.
Akifungua
mkutano kama huo mkoani Kilimanjaro, Makamu Mweneyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk
amesema zoezi hilo tayari limeshafanyika Kigoma, Tabora, Katavi, Geita,
Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma, Singida na
Zanzibar.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Bw. Kailima Ramadhan amesema Tume imeridhia kuongezeka kwa vituo 44 vya
kupigia kura ambavyo vinafanya idadi ya vituo vya kupigia kura nchini
kuwa 40,170 kutoka 40,126 vilivyokuwepo awali.
“Tume
imeridhia kufanyika kwa mabadiliko ya idadi ya vituo vya kuandikisha
wapiga kura kutoka vituo 40,126 hadi kufikia vituo 40,170 kwa kurejesha
vituo 44 vya Kata 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Vituo
39,753 vipo Tanzania Bara na 417 vipo Zanzibar,” amesema.
Hatua
hiyo ya Tume imetokana na amri ya Waziri wa Nchi, mwenye dhamana ya
TAMISEMI kupitia Tangazo la Serikali Na. 796 ya tarehe 06 Septemba, 2024
ambayo pamoja na mabadiliko mengine, imerejesha kata 11 za Halmashauri
ya Wilaya ya Ngorongoro ambazo zilifutwa hapo awali.
Kailima
amesema kwenye Mkoa wa Arusha Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura
wapya 224,499 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 ya wapiga kura 1,255,584
waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Ameongeza kuwa Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Arusha utakuwa na wapiga kura 1,480,083.
Amesema
kwa Mkoa wa Arusha kuna vituo 1,454 vitakavyotumika kwenye uboreshaji
kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 86 katika vituo 1,368
vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
Akiwasilisha
nada mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume, Bw.
Selemani Mtibora amesema kwa mkoa wa Kilimanjaro Tume inatarajia
kuandikisha wapiga kura wapya 180,540 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18
ya wapiga kura 1,009,726 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura.
“Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Kilimanjaro utakuwa na wapiga kura 1,190,266,” amesema.
Ameongeza
kuwa Mkoa wa Kilimanjaro una vituo 1,316 vitakavyotumika kwenye
uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 30 katika vituo
1,286 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
Wadau