Sambamba na ujenzi huo, Acp J. Omori alitaja miradi mingine ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya polisi vinayoendelea katika hatua mbalimbali ndani ya mkoa wa lindi.
miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Polisi daraja c na nyumba mbili za makazi ya askari kwenye kata ya Nandagala wilaya ya Ruangwa Milioni 164, ujenzi wa kituo cha polisi daraja c kwenye kata Kibutuka wilaya ya Liwale wa Milioni 115, ujenzi wa kituo cha polisi daraja c kwenye kata ya Somanga wilaya Kilwa wenye thamani ya sh Milioni 115, Ujenzi wa kituo cha Polisi daraja c kata Tingi wilaya ya kilwa wenye thamani ya sh Milioni115, Ukarabati wa kituo cha Polisi kwenye kata ya Naipanga wilaya ya Nachingwea Milioni 52, ukarabati wa kituo cha Polisi Nanjilinji kwenye kata ya nanjilinji wilaya ya kilwa Milioni 15.
Aidha, Mhe. Telack ametumia jukwa hilo kuwaomba viongozi wa dini kuwaombea watoto ambao wapo katika hatari ya matendo ya ukataili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili.