Rais wa Benki ya Dunia (WBG), Bw. Ajay Banga, akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao kama “Mission 300”, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unatarajiwa kuwa utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 inafanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kufikia 35 na utajadili namna ya upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo mwaka 2030.
Rais wa Benki ya Dunia (WBG), Bw. Ajay Banga (katikati), akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao kama “Mission 300”, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi (kulia). Mkutano huo unatarajiwa kuwa utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 inafanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kufikia 35 na utajadili namna ya upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo mwaka 2030.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es
Salaam)