Na Khadija Kalili
Michuzi TV
Benki ya NMB jana imetoa zawadi  pesa  zenye thamani  ya Mil.200 kwa washindi  zaidi ya 1,700 kupitia promosheni   ya  Mastabata.
Akizungumza   katika mkutano uliofanyika  tarehe 30, 2025 katika Ofisi  za NMB Bagamoyo Mkoani Pwani Meneja Huduma wa tawi hilo Mapesa Agrey Mapesa amesema kuwa  huu ni msimu wa sita wa   promosheni hiyo ya Mastabata.
Msimu huu wa sita  promosheni  ya  Mastabata ya kibabe  imedumu kwa miezi mitatu huku washindi zaidi ya 2,000 wamepatikana” amesema Mapesa.
Katika fainali ya droo ambayo tumepanga ifanyike tarehe 12 Februari 2025 tunatarajia kutoa zawadi   zenye thamani ya Mil.300  pia kupata washindi watano ambao watagharamiwa na Benki ya NMB  kwenda mbungani  kuona wanyama na wenza wao huku  wakilipiwa gharama zote kula kulala na mengineyo” amesema Mapesa.
Washindi wengine watano watajishindia kiasi cha Mil.4 kila mmoja ambazo zitakua kwa ajili ya kuwalipia ada watoto wao ama kwa matumizi binafsi” amesema Meneja  huyo wa Tawi la NMB  Bagamoyo.
Katika droo hiyo imekua ikitoa zawadi ya fedha taslimu kiasi cha  Sh.100,000  papo kwa hapo  kwa washindi 40 kila wiki.










