Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kuzindua mgahawa wa KFC katika Stesheni ya SGR ya Magufuli jijini Dar es Salaam leo Februari 11, 2025.
Waziri wa Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa kikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mgahawa wa chakula wa KFC katika stesheni ya John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam leo Februari 11, 2025. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dough Works Limited, Vikram Desai, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akiomba chakula kimtandao kutoka mgahawa wa KFC uliofunguliwa katika Stesheni ya SGR ya Magufuli jijini Dar es Salaam leo Februari 11, 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dough Works Limited, Vikram Desai akizungumza mara baada ya kuzindua mgahawa wa KFC katika Stesheni ya SGR ya Magufuli jijini Dar es Salaam leo Februari 11, 2025.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa mgahawa wa KFC katika Stesheni ya SGR ya Magufuli jijini Dar es Salaam leo Februari 11, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa mgahawa wa KFC katika Stesheni ya SGR ya Magufuli jijini Dar es Salaam leo Februari 11, 2025.
Picha za pamoja.
KAMPUNI ya Dough Works Limited (DWL) imefungua mgahawa wake wa 11 wa KFC katika Stesheni ya Reli ya Standard Gauge (SGR), ya Magufuli, na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma ya Chakula, kuongeza ajira, lakini pia kuchochea ukuaji wa uchumi.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewaasa kampuni ya Dought Works Limited (DWL) kufungua migahawa ya chakula katika Mkoa wa Dodoma pamoja na Morogoro ili kurahisisha upatikanaji wa chakula kwa wananchi wanaosafiri kutoka Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.
Hayo ameyasema leo Februari 11, 2025 wakati wa kufungua mgahawa wa KFC wa 11kwenye kituo cha SGR cha Magufuli kilichopo jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa ili kuchochea uchumi na kuongeza ajira kwa vijana.
Amesema kuwa kwa kuwa Dar es Salaam kunamigahawa mingi kwa hiyo kufungua mgahawa huo Dodoma utakuwa na wateja wengi zaidi kuliko Dar Es Salaam.
“Kufunguliwa kwa KFC katika Kituo cha SGR Magufuli ni uthibitisho wa maendeleo ya haraka ya miundombinu ya Tanzania na jukumu la uwekezaji wa sekta binafsi katika kuimarisha huduma za umma. Ushirikiano huu sio tu unatoa urahisi kwa wasafiri lakini pia hutoa ajira na kusaidia biashara za ndani,” amesema Prof. Mbarawa
KFC Tanzania inajivunia kufungua tawi lake jipya zaidi katika Stesheni ya Magufuli ya kuashiria hatua muhimu katika safari ya Tanzania kuelekea miundombinu ya kisasa na maendeleo ya kiuchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dough Works Limited, Vikram Desai amesema “Katika kampuni ya Dough Works Limited, tumejitolea kukuza uchumi kwa kutengeneza ajira na kutoa uzoefu wetu wa kutengeneza chakula chenye viwango vya juu kabisa. Chombo hiki kipya cha KFC katika Kituo cha SGR Magufuli kinaendana na maono yetu ya kuleta ubora na urahisi kwa Watanzania wengi huku tukisaidia wauzaji bidhaa na wafanyabiashara wa ndani. Amesema Desai
Uzinduzi wa mgahawa wa KFC katika Kituo cha Reli ya Kisasa (SGR) cha Magufuli, ni muhimu kwa abiria na kuhamasisha uwekezaji katika miundombinu yetu ya kisasa ya reli.” Bw. Masanja Kadogosa – Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Mradi wa SGR wa Tanzania unaongeza muunganisho wa kitaifa na kikanda, na kufanya usafiri kuwa salama, haraka na wa ufanisi zaidi. Kuongezwa kwa KFC katika Stesheni ya Magufuli kunaongeza uzoefu huu kwa kutoa chaguo la chakula chenye ubora wa hali ya juu kwa abiria wanaosafiri kati ya miji mikubwa kama vile Dodoma na Morogoro. Wasafiri sasa wanaweza kufurahia mlo wa haraka na wenye ladha nzuri kabla ya kupanda treni tayari kwa safari yao.
“Pamoja na maendeleo yanayoendelea ya miundombinu ya reli ya Tanzania, ni muhimu kuunganisha huduma za kiwango cha kimataifa ambazo huongeza urahisi na faraja kwa wasafiri. Tawi hili la KFC katika Kituo cha SGR Magufuli si mgahawa tu—ni ishara ya maendeleo, uvumbuzi, na uwezo unaokua wa kiuchumi wa Tanzania,” ameongeza
Mgahawa huo mpya utaongeza urahisi kwa wasafiri kupata huduma mbalimbali kama vile za chakula na vinywaji lakini pia kitatengeneza nafasi za ajira na huchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.
Mgahawa huo wa KFC upo katikati kitovu cha usafiri nchini Tanzania kwa sasa, unatazamiwa kuhudumia wafanyakazi wa SGR, wasafiri wa kila siku na wasafiri wa masafa marefu kwa milo yake mizuri na ya kuvutia.
Zaidi ya duka la vyakula vya haraka, mgahawa huu unawakilisha dhamira ya uvumbuzi, kuanzisha migahawa ya kujihudumia—ambayo ni ya kwanza kwa KFC nchini Tanzania—kuwaruhusu wateja kuagiza kwa ufanisi na kupunguza muda wa kusubiri.