Mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Shusho ameitambulisha brand yake mpya ya mavazi iliyopewa jina la Mama Mkwe Collection ambayo imezinduliwa Usiku wa Leo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete
Katika uzinduzi huo pia ametambulisha kampuni yake ya Duka la Nyuma ambalo litasaidia watu mbali Mbali kuweza kumiliki Nyumba kwa kulipia taratibu huku akimpongeza Rais Rasamia kumsaidia kupitia mkopo uliotolewa na serikali yake ndio umeweza kumsaidia yeye kufanya uwekezaje Mkubwa hivyo
“Nimeanza kuimba nikiwa na miaka 23, Nashukuru Mungu leo nina watoto na wajukuu, sijaja kuzindua album, Nimekuja kutangaza mavazi ya mwanamke wa Kiafrika,
“Mimi nimnufaika kwanza wa Mikopo, nilichukua mara ya kwanza na walipoona narejesha vizuri Nikachukua tena, baada ya hapo nilikaa chini na menejimenti yangu tukapata wazo na leo tunazindua Mama Mkwe Collection ambayo ni mavazi na Duka la Nyumba, hivyo tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kutuwezesha kupitia mikopo..” Christina Shusho
Katika uzinduzi huo walikuwepo watumishi wa Mungu kama Mwamposa, Wasanii wa filamu kama Irene Uwoya, Steve Nyerere, Wasanii wa Bongofleva kama Rayvanny, Msechu Bendi na wasanii wa Injili kama Bella Kombo, Paul Clement na wengine.
The post Christina Shusho aitambulisha brand yake mpya ya mavazi “Mama Mkwe Collection” first appeared on Millard Ayo.