Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa
nchini Ethiopia tarehe 14 Februari, 2025 kwa ajili ya kushiriki Mkutano
wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).
Pamoja na mambo mengine pia Mhe. Rais Dkt. Samia atashiriki mkutano wa
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika