Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele
akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika
Machi 01 hadi 07, 2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00
jioni kwa siku saba.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele
akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika
Machi 01 hadi 07, 2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00
jioni kwa siku saba.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika Machi 01 hadi 07, 2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni kwa siku saba.
Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume, Ndg. Stanslaus Mwita akiwasilisha mada wakati wa mkutano huo hayo.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele
(kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani
wakati wa mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika Machi 01 hadi 07,
2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni kwa siku
saba.
Na.
Mwandishi Wetu
Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuanza kwa mzunguko wa 12 wa
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utafanyika mkoani Morogoro
na sehemu ya mkoa wa Tanga kwa siku saba kuanzia tarehe 01 had 07 Machi, 2025.
Akifungua
mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Morogoro leo tarehe 17 Februari, 2025,
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa, Jacobs
Mwambegele amesema uboreshaji huo utafanyika kwenye mkoa huo na mkoani Tanga
kwenye halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga.
“Kwa
mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 12 kati ya
mizunguko 13 ya uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu wa 12 unahusisha Mkoa huu
wa Morogoro na Mkoa wa Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni,
Pangani na Mkinga,” amesema Jaji Mwambegele.
Amesema
mikoa 27 tayari imekamilisha zoezi hilo ambayo ni pamoja na Kigoma, Tabora, Katavi,
Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma na Singida.
Ameitaja
mikoa mingine kuwa ni Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini
Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe,
Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara.
“Mikoa
miwili ya Pwani na sehemu ya mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga,
Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi,
Lushoto na Muheza inatarajia kukamilisha zoezi hilo tarehe 19 Februari, 2025,”
amesema.
Wakati
huohuo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndugu. Kailima Ramadhani amesema Tume
inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 302,752 mkoani Morogoro sawa na
ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 1,612,952 waliokuwepo kwenye daftari
la wapiga kura mwaka 2020.
“Tume
inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Morogoro utakuwa na wapiga kura 1,915,704.
Idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao
walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa
Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza
kujiandikisha,” amesema.
Ameongeza
kuwa Mkoa wa Morogoro una vituo 2,816
vitakavyotumika kwenye uboreshaji wa daftari ikiwa ni ongezeko la vituo 112
katika vituo 2,704
vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.