Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Florent Kyombo imewasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kutembelea Taasisi za Muungano.
Kamati hiyo inaratajia kutembelea na kupokea taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na taasisi hizo ambazo ni Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na Tume ya Pamoja ya Fedha.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameongoza ujumbe wa Serikali.