Na Khadija Kalili, Michuzi TV
KIWANDA Cha Doweicare kilichopo eneo la Lulanzi Picha
yandege Wilayani Kibaha wametoa mchango wa fedha ikiwa katika kuchangia ujenzi wa kalavati.
Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bob Chaing amesema kuwa wamekabidhi kiasi cha Sh.500,000 kwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa ya Lulanzi huku akisisitiza na kusema kuwa wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii Wilayani hapa na ndani ya Mkoa wa Pwani kwa ujumla.
Doweicare ambao ni wazalishaji wa taulo za kike (Softcare Sanitary Pads) tunayofuraha kubwa kurejesha kwa jamii japo itaonekana ni kidogo lakini tunayorekodi ya kuchangia huduma nyingi ” amesema Chaing.
Amesema kuwa wanapokuwa na nguvu wanachangia na hata pindi daraja litakapokamilika watakuwa sambamba.
Akizungumza leo tarehe 5 Februari 2025 Mwenyekiti wa Mtaa wa Lulanzi. Thomas Shilole amewaeleza Waandishi wa Habari kuwa wanashukuru kwa mchango huo kwani eneo hilo limekuwa korofi kupitika hasa nyakati za mvua.