



Benki ya Exim Tanzania imeandaa futari maalum Tanga na Zanzibar, ikikusanya pamoja wateja wake, viongozi wa dini, na wadau wakuu kwa jioni ya shukrani, mshikamano, na tafakari katika mwezi huu mtukufuwa Ramadhan.
Hafla hizi zilitoa fursa ya kusherehekea maadili ya ukarimu, uadilifu, n amsaada wa kijamii—ambayo yanawiana na misingi ya Uislamu pamoja na dhamira ya Benki ya Exim ya kuwawezesha watu kifedha na kuwajibika kwa jamii.
Hafla hizi za futari ni sehemu ya dhamira pana ya Benki ya Exim ya kushirikiana na wateja wake na kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii. Mbali inkutoa huduma za kifedha zinazozingatia misingi ya sheria, benki hiyo inaendelea kuwekeza katika program zinazolenga kuinua biashara na watu binafsi huku ikikuza maadili ya kibenki yenye uwazina uadilifu.
Benki ya Exim inaendelea kuwa mshirika wa kuamini kwa kifedha, ikihakikisha kuwa huduma zake zinakidhi mahitaji ya wateja wake, bali pia zinachangia ustawi wa jamii kwa ujumla.