Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema kuwa vyuo VETA vinatambua makundi mbalimbali yenye uhitaji.
Makundi yenye mahitaji maalum kwenye mikakati ya VETA yamepewa kipaumbele katika kuwapatia mafunzo ya ujuzi kwani ulemavu si kikwazo katika kupata elimu pamoja na hakuna sababu ya jamii kuwafungia ndani na badala yake watumie fursa ya kuwapeleka vyuo vya VETA kupata ujuzi nchi nzima
CPA Kasore aliyasema katika Maonesho na Kongamano la Mavazi, Nguo wakati alipukutana na Mlemavu wa Viungo Riziki Ndumba ambaye licha ya changamoto zake ameweza kusimama kwa kujiajiri katika fani ya ushonaji.
Amesema Riziki amepata mafunzo ya Ujuzi na Ufundi katika Chuo cha VETA Songea ambapo amehitimu na kuanza kujitegemea kwa kuwa na ofisi yake Mjini Songea.
Aidha amesema miaka 30 ya maadhimisho ni mafanikio pamoja na kuwafikia watu wenye mahitaji wakapata ujuzi na kuondokana changamoto zao na kuanza kufikiria kutengeneza uchumi.
Mhitimu Riziki anaishukuru VETA katika malezi na kupata ujuzi unaomsaidia katika maisha yake kwa sasa na baadae kuendeleza fani hiyo.
Amesema kuwa mategemeo yake ni kuongeza mashine na kuajiri vijana wenzake katika fani hiyo.