Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Serikali kupitia uwekezaji wa Samia Commercialization Fund,imewekeza sh bilioni 2.3,kwa ajili ya kuwapa wabunifu wa Kitanzania fursa ya kuingiza bunifu zao sokoni,kitendo ambacho kimesaidia kuondoa changamoto ya kukosekana na dhamana ili kupata mitaji.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Dkt Amos Nungu,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.
Amesema kwa usimamizi thabiti wa serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, COSTECH imefanikiwa kuandaa mifumo ya usimamizi wa tafiti kwa kutumia teknolojia za kidijitali kupitia mradi wa HEET, pamoja na kuanzisha vigoda vya utafiti katika vyuo vikuu kama SUA na NM-AIST kwa ufadhili wa shilingi bilioni 4.7.
Amesema kwa kipindi cha miaka minne (2021/22 hadi 2024/25), COSTECH iliendelea kutekeleza kazi zake kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake pamoja na vipaumbele ilivyojiwekea.
DKt Nungu amefafanua zaidi ya kuwa,kwa mafanikio haya,Tanzania inajiweka katika nafasi ya ushindani wa kimataifa katika nyanja ya sayansi na teknolojia katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo amesema pia,uwekezaji huu si wa kawaida, bali ni hatua ya kimkakati inayoonesha kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu ameleta mapinduzi katika sekta ya sayansi na teknolojia, ikiwa ni kielelezo cha uongozi wenye dira na maono makubwa kwa taifa.
Amesema katika kuimarisha miundominu ya utafiti, pamoja na kutoa fedha kwa vyuo vikuu, Serikali imetoa shilingi bilioni tisa ili kuhakikisha kuwa jengo la COSTECH linafanyiwa ukarabati ikiwemo pia kujenga jengo jipya hapa Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH amesema, majukumu ya COSTECH yamejikita katika maeneo makubwa saba yanayojumuisha kuratibu, kukuza na kuendeleza utafiti,kushauri Serikali kuhusu masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu,kukusanya, kuhifadhi na kusambaza taarifa za sayansi,
Katika hatua nyingine kongano Bunifu na Mapinduzi ya Teknolojia Chini ya uongozi wa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan, COSTECH imeanzisha na kuziwezesha kongano nane bunifu katika mikoa ya Kigoma, Geita, Mafia, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Singida na Pemba ili kusaidia sekta ya viwanda na kilimo.
Anasema Miradi hiyo imewezeshwa kwa ufadhili wa shilingi milioni 750, kuhakikisha teknolojia bora zinatumika katika kuboresha uzalishaji wa mafuta ya mawese, dhahabu.