OR-TAMISEMI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeielekeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mjini kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa uzio katika madarasa ya awali ya Shule ya Msingi Uyole.
Maelekezo hayo yametolewa katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo na
Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye Mbunge wa Kilindi, Mhe. Omary Kigua kwa niaba ya Mwenyekiti wa LAAC, Halima Mdee.
Amesema “Afisa Masuhuri hakikisha uzio katika madarasa ya awali uwe umejengwa kabla ya kukamilika kwa mwaka wa fedha 2025/26, na taarifa ya ujenzi huo iwasilishwe kwa CAG kwa ajili ya mapitio.”
Pia, Amesema Kamati imeelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa jengo la kufulia katika Kituo cha Afya Itamba unakamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha.
Naye, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa serikali kupitia TAMISEMI itafanyia kazi mapungufu yote yaliyoainishwa na Kamati ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika kwa manufaa ya wananchi.
Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na Ujenzi wa machinjio ya kisasa Ngelewala, Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Mkondo Mmoja Uyole na Ujenzi wa Kituo cha Afya Itamba ambapo kamati imesisitiza ikamilike kwa wakati ili kuboresha huduma kwa wananchi wa Iringa.