Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu akizungumza kwenye kikao cha wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu pamoja na wanasheria Jijini Mwanza

Wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu pamoja na wanasheria wakiwa ukumbini
…..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Serikali imezitaka Halmashauri kupitia Idara za Utawala na Rasilimali Watu Nchini kuhakikisha wanawasilisha michango ya watumishi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuepuka kukwamisha mafao ya watumishi pindi wanapostaafu.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jumanne Machi 18, 2025 Jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu kwenye kikao kazi cha wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu pamoja na wanasheria kilicholenga kuwakumbusha sheria na kanuni za utumishi wa umma.
Ameeleza kuwa wamekuwa wakipokea barua nyingi za ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi ambayo tayari yamekwisha kutolewa ufafunuzi wa maelekezo hivyo kupelekea mambo hayo kuonesha ni moja ya sababu ya watu kutowajibika ipasavyo katika kusimamia sera, kanuni, taratibu na Sheria zilizowekwa.
Kikao hicho kimewakutanisha Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu pamoja na Wanasheria kutoka mikoa tisa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hilda Kabisa ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwanamna inavyohakikisha watumishi wake wanakipwa malimbikizo yao.
Naye Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Silas Kapinga amekiri kuwepo kwa tatizo la uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.