Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele
akimkabidhi kadi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Abubakari Majuto mkazi wa
Mzambarauni Kata ya Gongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa
viungo alijitokeza kujiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi
Mzambarauni leo Machi 18, 2025.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele
akimkabidhi kadi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Abubakari Majuto mkazi wa
Mzambarauni Kata ya Gongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa
viungo alijitokeza kujiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi
Mzambarauni leo Machi 18, 2025.Wananchi
wakiwa katika moja ya vituo Jijini Dar es Salaam kujiandikisha na
kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele
leo Machi 18, 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa
zoezi hilo katiuka siku ya pili.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele
leo Machi 18, 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa
zoezi hilo katika siku ya pili. Mjumbe
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina
Omari, leo Machi 18, 2025, ametembelea na kukagua vituo vya
kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, katika Jimbo la
Temeke, lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina
Omari, leo Machi 18, 2025, ametembelea na kukagua vituo vya
kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, katika Jimbo la
Temeke, lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.Mjumbe
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe
18 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura
Jimbo la Ilala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuona zoezi la
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.
Mjumbe
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe
18 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura
Jimbo la Ilala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuona zoezi la
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.
Wananchi
wa Kata ya Kivule jijini Dar es Salaam wakiwa wamejitokeza kwa wingi
kujiandikisha na kuboiresha taarifa zao katika kituo cha Ukooni Kivule.
Na. Mwandishi Wetu
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema itaongeza mashine za BVR na
watendaji katika vituo ambavyo vimebainika kuwa na watu wengi ili
kufanikisha uandikishaji na uborteshaji wa taarifa katika Daftari la
Kudumu lka Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs
Mwambegele ameyasema hayo leo Machi 18, 2025 katika siku ya pili ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati akikagua vituo
Mkoani Dar es Salaam.
“Leo
katika siku ya pili ya zoezi nimetembelea vituo vya uboreshaji na
waliojitokeza wamekua wengi mmno kiasi kwamba vifaa vinaonekana ni
vichache, nimeagiza vifaa kwamba viongezwe na vituo viongezwe ili kuweza
kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Mhe. Jaji wa Rufani
Mwambegele.
Jaji
Mwambegele akiwa katika Kituo cha Lukooni Chanika Jijini Dar es Salaam
alishuhudia uwepo wa wananchi wengi waliojitokeza kwaajili ya kuboresha
taarifa zao na kujiandikisha na kutoa maagizo ya kuongezwa kwa mashine
za BVR katika kituo hicho.
“Hapa
Lukooni eneo la Chanika katika Wilaya ya Ilala kulikua na kituo kimoja
katika siku ya kwanza, lakini baada ya kubaini kwamba watu wanakua ni
wengi na wanatumia muda mrefu nikaagiza vifaa viongezwe na leo nimepita
bado nimeona BVR mbili hazitoshi kwahiyo nimeagiza ziongezwe ili kuweza
kukabiliana na changamoto hii,” aliongeza Jaji Mwambegele.
Aidha,
Jaji Mwambegele amepongeza wananchi wote waliojitokeza kwa wingi
kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika siku za mwanzo za zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu kwani kufanya hivyo kunawezesha wao
kukamilisha zoezi hilo ndani ya siku saba kama ilivyopangwa.
Nae
afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es Salaam, Faraja Nakua amesema
katika Majimbo matatu yaliyopo katika Halmashauriu ya Jiji la Dar es
Salaam yenye majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea zoezi linakwenda vyema
na wao wamejipanga kufanikisha zoezi hilo.
“Nizidi
kuwahamasisha wananchi wa Majimbo ya Ukonga, Ilala na Segerea Jijini
Dar es Salaam kuendelea kujitokeza kwa wingi na sisi tumejipanga
kutekeleza zoezi hili kama ambavyo Tume imeagiza na vifaa tulivyotakiwa
kuongeza vipo tutavipeleka katika maeneo yote yenye changamoto,” alisema
Nakua.
Nae Atness
Shayo mkazi wa Ukonga Mzambarauni na Hassan Said Mmanga wa Chanika
wamepongeza ujio wa zoezi hilo kwani walipoteza kadi zao za mpiga Kura
na sasa wameoata kadi zao mpya zitakazoweawezesha kupiga Kura katika
Uchaguzi Mkuu baadae mwaka huu.
Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi inataraji kuandikisha Wapiga Kura wapya
643,420 mkoani Dar es Salaam ambapo jumla ya vituo 1,757 vinatumika
kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 96
katika vituo 1,661 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka
2019/20.
Aidha Tume
imejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za
kuandikishwa wanaandikishwa kwani BVR zaidi ya 5,000 na watendaji wa
kutosha wapo kwaajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Tume
imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 29. Kwa mujibu wa
ratiba, leo Tume inaanza uboreshaji katika mzunguko wa 13 ambao ni
mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha
Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Kailima
amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam Tume inatarajia kuandikisha wapiga
kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga
kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Tume
inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na
wapiga kura 4,071,337 idadi ambayo inaweza kuongezeka kwa kuwa
inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa
wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa
sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha.
Zoezi
la uboreshaji wa Daftari linahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao
ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza
umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kutoa kadi mpya
kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kutoa fursa
kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina
na taarifa nyingine.
Uboreshaji
wa Daftari pia unahusu kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye
Daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au
jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za
kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuukana uraia wa Tanzania na kifo.