Na Mwandishi Wetu.
SHARIF Mohammed alhatim, amewaka Murid, waendelee kusimama kwenye Twarika, maana ndiyo iliyoongoza kuwaweka Waislam karibu duniani kote.
Akizungumza mara baada ya hafla maalum ya Iftar iliyofanyika jana makao makuu ya Taasisi ya Almasjid Zawiyati Alqaadiriya Tanzania (AZAT) Sheikh Sharif Mohammed Alhatim kutoka Mombasa Kenya, amesema ni jambo jema kuendelea kusimama ulipoona kufaa kuhudumu.
Amesema Twarika imesambaa sehemu nyingi na ni moja ya viunganishi vizuri kwenye uslamu.
Ameingia Tanzania hiyo jana na moja kwa moja akaamua ajiunge na Wana Kadiria hao wa Mabibo kwa ajili ya kufuturu pamoja ikiwa ni sehemu ya kukuza na kuendeleza Twarika.
“Nimekuja leo mchana (jana), lakini moja kwa moja nikaamua nije huku kufuturu na kukutana na ndugu zangu wa Twarika, nimefurahi sana kuona mlivyoungana na muendelee kuipambania Twarika, maana ni kiunganishi kizuri kwa Waislam”.
Akizungumza kwa niaba ya Wana Twarika Sheikh Mahmoud Waziri ambaye ndiyo Sheikh Mkuu wa Taasisi hiyo, amemshukuru Sheikh Sharif kwa ujio wake.
Amesema wamepata furaha kubwa kwa Taasisi yao kwa ujio wake kwao na kwamba jambo ni jambo la faraja kupata kiongozi hiyo wa dini na kutembelea tasisi yao.
“Tumefurahi sana kupata ujio wake, tunakukaribisha tena, vile vile tunaomba usiishie kuja leo tu, nasi tunahitaji kuja Kenya tujifunze zaidi elimu yetu ya dini ya Kiislam.”amesema.
Aidha Waziri amesema kwenye taasisi yao wamejaaliwa kupata wageni tofauti tofauti, ikiwa ni pamoja na Mufti wa Tanzania Sheik Dk.Aboubakari Zuberi na kuongeza taasisi hiyo ina zaidi ya Murid 3000 na imeendelea kuipambania na kusimama taratibu zote za kizawia duniani.