Wadau
mbalimbali na Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kudhamini
Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika katika mikoa 26 nchini
Akizungumza
na waandishi wa Habari April 2,2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotion , Alex Msama amesema tamasha hilo halitakuwa
na kingilo ili kila mtanzania aweze kushiriki kwenye kuliombea taifa
huku maandilizi yakiwa yanaendele vizuri
Msama ameongeza kuwa
tamasha litaanzia katika mkoa wa Dar es salaam na kwenda mikoa mingne na
limehusisha Wachungaji, Maskofu wa mikoa mbalimbali katika kuhakikisha
wanaombea amani kulekea uchaguzi Mkuu.
Aidha amesema waimbaji mbalimbali wakubwa kutoka nje ya nchi na Ndani ya nchi watakuwepo kwenye tamasha la Kuombea Uchaguzi.
“
Tutatangaza tarehe na eneo ambalo tamasha hili litafanyika hivi
karibuni kwa mkoa wa Dar es salaam ambapo tamasha hili ndipo litakapo
anzia” amesena Masama
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Barazaa
Makanisa ya Kipenteksote Mkoa wa Dar es salaam, Mch Emmanuel Mwasota
amesema tamasha hilo lipo kwajili ya Maombi ya Kuombea uchaguzi Mkuu kwa
kuungana kwa pamoja kwa waumi wote wa madhehebu yote kuiombea nchi
yetu, viongozi , wabunge, madiwa na Rais wetu ili chaguzi uweze kupita
kwa amani
“Sisi tumesema ya kwamba tutashikama kwa pamoja na
taarifa hizi zinaenda kila mahali kwa makanisa, wachungaji, maskofu na
waubiri wa aina mbalimbali tutakuwa kwa Pamoja kwaajili ya kuhakikisha
tunaombes nchi yetu ipite salama kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka
huu”
Ameongeza kuwa uchaguzi unaweza kusabisha nchi inaweza
ikapasuka kama raia wake wasipokuwa wazalendo hasa kwa upande wa amani
kwajili ya kuombea nchi na viongozi wetu ambao wanatuongoza katika
maswala ya nchi yetu na sisi tunahitaji amani na maombi ili tuweze
kuvuka kwenye uchaguzi kwa amani