Na Ali Issa Maeleza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesema Serikali imeandaa utaratibu wa kuwaombea Waasisi na voingozi wa Serikali walioitumikia nchi kwa upendo mkubwa na maslahi mapana ya wazanzibar ili kukumbuka mchango walioutoa katika uhai wao.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa na wanafamilia kumuombea dua aliyekuwa Rais wa awamu ya Pili Marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi huko Nyumbani kwa Marehemu Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi amesema kuwa dua hiyo ni mfulilizo wa utaratibu uliopangwa wa kuwakumbuka na kuwaombea waasisi waliopigania nchi na kuikomboa kwa kuwa huru na amani.
Mhe. Hamza amesema utaratibu huo utaendelea kuwaombea rehema kwa Mwenyezi Mungu waasisi wote waliotangua kwa moyo wao wa ushujaa kwani mazuri walioyafanya ndio yaliowaunganisha wazanzibar na kuwa Taifa moja lenye upendo.
Nae Kiongozi wa Familia ndugu wa marehemu Rajab Abuod Jumbe akitoa neno la shukurani kwa Serikali na watu waliohudhuria hapo na kumshukuru Rais Hussen Mwinyi kuendeleza utaratibu huo kwa wanafamilia wamefarjika kuungana na wenzao viongozi wa Serikali na wananchi kumuomea dua Mzee wao.
Katika dua viongozi na wananchi mbali mbali walihudhuria wakiwemo wanafamilia viongozi wachama na Serikali wakiongozwa na Hemed Saleh Ali Mjumbe kutoka Mahkama ya Kadhi Mjini Zanzibar.