Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akishuhudia utilianaji Saini wa Makubaliano kati Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company -TFC) na Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa Zao la Tumbaku,hafla iliyofanyika leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma.
……
Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company -TFC) imesaini Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa zao la Tumbaku.
Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Gerarld Mweli pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Bw. Samuel Mshote.
Mara baada ya kushuhudia utilianaji Saini ya Makubaliano hayo, Mhe. Bashe amesema kuwa ndani ya makubaliano hayo yapo makubaliano ya kujenga kiwanda cha mbolea hapa nchini lengo ni kurahisisha upatatikanaji wa Mbolea kwa wakulima wa zao hilo.
Waziri Bashe amesema wamekubaliana na UFCL kwa ajili ya kujenga Kiwanda cha kuzalisha tumbaku ambapo ameeleza mchakato wa awali tayari umeishafanyika na shughuli zingine za utekelezaji zinaendelea.
Amesema wanaangalia eneo ambalo litawekwa Kiwanda hicho huku akidai watashirikiana kwa pamoja na sekta binafsi na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).
Aidha, Waziri Bashe amewapongeza wakulima wa zao la tumbaku kwa kazi nzuri wanayofanya pamoja na vyama vya ushirika ambapo amedai Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano na wataufungua mpya msimu wa zao hilo hivi karibuni.
Katika hatua nyingine, Waziri Bashe ametoa wiki kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bw. Joel Laurent kuhakiki majina ya wakulima wa zao la tumbaku ili waweze kupatiwa ruzuku zao.
Amesema tayari Serikali imeishatoa zaidi ya Sh bilioni 13 lakini kumetokea changamoto ya majina kwa wakulima.
“Nimewapa siku saba wahakiki majina ya wakulima ili wakulima wapate fedha yao ya msimu uliopita,” amesema Waziri Bashe.
Waziri huyo wa Kilimo amesema mpango wa Serikali kwenye ruzuku itaendelea kwani ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kuhusu Mbolea ya kupandia amesema tayari TFC inazo tani elfu 14 na mbolea yote ya shambani tayari imezalishwa.
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akizungumza mara baada ya kushuhudia utilianaji Saini wa Makubaliano kati Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company -TFC) na Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa Zao la Tumbaku,hafla iliyofanyika leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akishuhudia utilianaji Saini wa Makubaliano kati Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company -TFC) na Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa Zao la Tumbaku,hafla iliyofanyika leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma.