Na Diana Byera,Missenyi.
Ikiwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imeingia siku ya Nne katika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, wataalamu wa kisheria na waratibu wa kampeini hiyo wametoa Elimu ya masuala ya urithi kwa wanawake ambayo inalenga kuwaelimisha wanawake kurithi Mali na Kuandika Wosia wa kurithisha
Kurithi shamba na kjurithisha kwa wanawake ni moja ya changamoto zilizojitokeza mpaka sasa kwenye mikutano mbalimbali ambayo inaratibiwa na waratibu wa kampeni ya Kisheria ya Mama Samia.
Baadhi ya wanawake waliofika katika mikutano hiyo kuwasilisha changamoto za kisheria ni pamoja na wanawake ambao hawajapata haki ya kurithi Shamba na Kuandika Wosia hata kama wamefiwa na wanaume zao ,au wameachiwa na ndugu zao .
Sara kaloli mkazi wa Wilaya ya Missenyi amefikisha shauli lake mbele ya timu ya wataalam wa kampeni hiyo na kudai kuwa angetaka kupata haki yake ya kupata shamba aliloachiwa na baba yake, lakini mara nyingi amekutana kauli za mwanamke hawezi kurithi Shamba, hivyo ikasababisha kukosa haki yake ya Msingi ambapo timu ya wataalamu wa kampeini wilayani Missenyi Wameanza kushughulikia swala lake.
Kutokana na suala hilo kujitokeza Wakili wa kujitegemea na mjumbe wa kamati hiyo Jofrey Binamungu ametumia saa nzima akitoa Elimu kwa wananchi wa Kijiji Cha Bukabuye kata Bwanjai wilaya ya Missenyi juu ya Haki ya kisheria ya mwanamke kurithi Mali na kuacha Wosia kwa watu anaotaka kurithisha;’
“Mwanamke anapaswa kurithi Mali ,kulithishwa ,Kuandika Wosia wa kuwarithisha wengine, leo wanawake wengi hawapewi ardhi ni kama wameshikizwa tu eneo la kulima lakini akitaka kufanya maamuzi juu ya aridhi yake migogoro inaibuka kuwa kero na kuwanyika haki wanawake Kurithi”alisema Binamungu
Afisa Aridhi na mipango miji na vijiji wilayani Missenyi Deliqueen Lyimo kupitia kampeni ya msaada wa Mama Samia anasema kuwa Kwa mwezi migogoro ya kisheria inayoletwa na wanawake kunyanganywa Ardhi kwa mwezi inafikia 12_15
Anasema kuwa Uwepo wa kampein ya msaada wa Kisheria ambayo imeangazia vijiji vya pembezoni wilayani Missenyi ,inayotoa Elimu ya kutosha juu ya msaada wa Kisheria itatoa mwanga mzuri wa wanawake kumiliki Ardhi kisheria na kufanya uwekezaji
Kampeini ya Msaada wa Kisheria ya mama Samia inaendelea kuwakunsanya mamia ya wananchi wa vijiji vya pembezoni wilayani Missenyi ambao wanapata faida ya kupata Elimu ya maswala yote ya kisheria, kuleta changamoto zao za kisheria,kupatiwa Suluhu ya kesi zao pamoja na kupata mawakili.