
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Masuala ya Utawala na Uendeshaji wa Benki ya Dunia, Bi. Anna Bjerde, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, Dkt. Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa mchango mkubwa wa maendeleo ya Tanzania kupitia miradi mbalimbali inayopata fedha kutoka Taasisi hiyo pamoja na kuonesha nia ya kusaidia ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR). (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C, Marekani)