
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia akimkabidhi zawadi ya TASAC Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Erasto Sima wakati wa Bodi hiyo ilipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika ziara ya Bodi mkoani humo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Erasto Sima akitoa taarifa kwa Bodi ya TASAC ilipotembelea ofisi hiyo kwa ziara ya bodi hiyo mkoani Kagera.
Bodi ya TASAC ikiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia akimkabidhi zawadi ya TASAC Mwenyekiti wa umoja wa usafirishaji Abiria na Mizigo Bumbile ,Jovinus tikyeba wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara katika Mwalo wa Lwazi wilayani Muleba mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa CCM Kata Kikuku William Bhangalo akizungumza kuhusiana na changamoto katika mwalo wa Lwazi wakati bodi ya TASAC ilipofanya ziara katika mwalo Lwazi wilayani Muleba mkoani Kagera.
Bodi ya TASAC ikipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Samaki cha Pride of Nile Hamza Mstapha namna wanavyochakata samaki hadi hatua ya kusafrisha kwa njia ya Bahari.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia akizungumza na wasafirishaji Bandari Magarini hawapo pichani wakati bodi ilipotembelea Bandari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Wakili Leticia Mutaki akizungumza kuhusiana na mikakati ya TASAC katika Bandari ya Magarini wakati Bodi ya TASAC ilipofanya ziara katika bandari hiyo.
Na Mwandishi wetu, Muleba
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala Meli Tanzania (TASAC), Nahodha Mussa Mandia amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha bandari zote nchini pamoja mialo ya Uvuvi ili kuongeza huduma za maendeleo kwa wananchi.
Nah.Mandia ameyasema hayo wakati Bodi hiyo ilipotembelea Bandari ya Magarini na Mwalo wa Lwazi katika Wilaya Muleba mkoani Kagera.
Amesema kuwa kama wadhibiti kazi yao kuangalia usalama wa Bandari, Mialo ya Uvuvi pamoja na shughuli zinazofanyika katika maeneo hayo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na salama ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa.
Nah.Mandia amesema kuwa miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali inatokana na rasilimali zilizopo kwa sasa na maeneo ambayo bado serikali inaendelea kufanyia kazi na kuwataka wananchi kuwa na subira huku wakiendelea kufanya shughuli zao.
Diwani Kata ya Kikuku Abdul Hassan amesema changamoto yao katika Mwalo wa Lwazi ni kukosekana kwa Ghati ya kuegeshea vyombo vya usafiri maji na kuomba kwa Serikali kutatua changamoto hiyo ambapo itasaidia kuongeza vyombo vya usafiri wa majini vinavyohudumia wananchi wa visiwa mbalimbali.
Amesema kuwa ziara ya Bodi ya TASAC ni moja ya njia ya Serikali kuwafikia wananchi kuwasikiliza na kushauriana ili kupata mwanga katika utatuzi wa changamoto zao. Amewaomba wananchi waendelee kuwa na imani ya Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi yake katika kutatua changamoto kwa wananchi wake na kuwaletea maendeleo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji wa Bandari ya Magarini amesema kuwa wanaishukuru TASAC kwa kuwapa elimu ya usalama wa vyombo vya majini ambapo wanaendelea kuwa kujisimamia kutokana na elimu hiyo.