
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Uwekezaji katika Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Investment Funds (CIF), Bi. Tariye Gbadegesin, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe, ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia ya mwaka 2025, inayofanyika jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo wamejadiliana masuala kadhaa kuhusu jinsi Mfuko wa CIF unavyoweza kusaidia juhudi za Tanzania katika kutekeleza Mpango wa Nishati (Energy Compact) na kuendeleza vipaumbele vya matumizi ya Nishati safi.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C, Marekani)