NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mhe.Sylvestry Koka amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitano kwa mwaka 2020/2025 ameweza kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ambayo yametokana na juhudi zake binafsi pamoja na fedha ambazo zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Koka ameyabainisha hayo wakati wa mkutano mkuu maalumu wa Jimbo la Kibaha mjini wa utekelezaji wa ilani ya chama kwa kipindi cha miaka mitano kwa mwaka wa 2020 hadi 2025 katika nyanja mbali mbali.
Koka amesema kwamba kitendo cha kuwa na Rais msikivu kimekuwa chachu ya maendeleo katika Jimbo la Kibaha mjini ambapo kero katika sekta mbalimbali zimetatuliwa na hivyo kuwafanya wabunge kumsaidia kwa urahisi utekelezaji wa ilani ya Chama.
“Raisi wetu ni mama msikivu anapoelezwa shida za wananchi hachelewi tutoa maelekezo ya utatuzi wa haraka kwa maendeleo yaliyopatikana kwenye Jimbo letu tuna kila sababu ya kumpa kura za heshima muda utakapofika,” amesema.
Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amesema chama hicho kinasimamia utekelezaji wa ilani ambapo miradi mbalimbali umetekelezwa kwa fedha kutoka Serikali kuu na mapato ya ndani.
Awali Katibu wa CCM Kibaha mjini Isack Kaleiya alisema wanaendelea kusimamia taratibu na kanuni za chama na kwa kila anayeenda kinyume na kanuni na taratibu za chama hatua zinachukuluwa kupitia kamati ya maadili.
Wajumbe zaidi ya 8000 wa CCM kutoka kata 14 wa ameshiiriki mikutano ya Jimbo iliyofanyika kwa siku tano kwa ajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani iliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka:




