Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kuimba Wimbo wa Taifa alipowasili kwenye ukumbi wa hoteli ya Gran Melia jijini Arusha, kuwa Mgeni rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Aprili 29, 2025. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, Ofisa Mtendaji Mkuu wa wa Jamii Afrika, Maxence Melo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Susan Ngongi Namondo. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)
Baadhi ya washirki wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani wakimpokea mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipoingia kwenye ukumbi wa hoteli ya Gran Melia jijini Arusha, Aprili 29, 2025. (Picha na OIfisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Gran Melia jijini Arusha, Aprili 29, 2025. (Picha na OIfisi ya Waziri Mkuu)