Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kuangalia huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wanazozitoa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima shinikizo la damu (BP) na kiwango cha oksijeni mwilini Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus aliyetembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mary Maganga akimsikiliza daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago alipofika kwenye banda la JKCI kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Dkt. Edith Rwiza akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.Picha na: Jeremiah Ombelo