Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili mkoani Njombe linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura ambapo mikoa 15 imeanza zoezi hilo litafanyika kwa siku saba kuanzia Mei 1 hadi 7, 2025. (Picha na INEC).
Wananchi wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa katika kiuo cha kujiandikishia wapiga Kura kilichopo ofisi ya Mtendaji Kihesa. Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi imeanza awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura katika mikoa 15 ya Tanzania bara kuanzia Mei Mosi hadi 07, 2025 unaokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali. (Picha na INEC).