Mkurugenzi wa Udhibiti huduma za usafiri majini TASAC Nelson Mlalali akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa Ukusanyaji na Utawanyaji wa Shehena jijini Dar es Salaam.
Mdau wa Ukusanyaji na Utawanyaji wa Shehena wa Kampuni ya Cuactus Eliud Haonga akizungumza kuhusiana na mada wanazopewa na TASAC katika mkutano wa wadau kwenda kutekeleza katika usimamiaji wa kanuni na sheria.
Mwenyekiti wa Chama cha Ukusanyaji na Utawanyaji wa Shehena Hawa Mohamed akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa mkutano TASAC ulioitishwa kwao katika kujadili mada mbalimbali zitazositawisha kazi zao.
*Yaweka mikakati ya kutoa elimu ya mara kwa mara wadau mbalimbali
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa wadau wa ukusanyaji na Utawanyaji wa shehena za mizigo bandarini kutoka ndani na nje ya nchi wametakiwa kutimiza wajibu wao kwa kufuata kanuni na taratibu katika kuleta maendeleo ya nchi pamoja biashara zao kukua.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Usafirishaji majini kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nelson Mlali wakati wa akifungua Mkutano wa Wadau wa ukusanyaji na Utawanyaji wa shehena za mizigo bandarini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mlali amesema kuwa mkutano huo lengo ni kiendelea kukumbushana kanuni katika ustawi kuendelea kuchochea maendeleo ya nchi.
Aidha amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kuimarisha miundombinu ya bandari ambapo wadau ukusanyaji na utawanyaji ni wadau wakubwa katika kutumia bandari pamoja na usafiri wa anga.
Hata hivyo amesema TASAC kukutana wadau katika kujenga na kuimarisha katika kukusanya na utawanyaji shehena kwa kufuata kanuni na sheria.
Amesema katika kufanikisha biashara kwa njia ya maji ni pamoja na kufikisha shehena sehemu husika kwa wakati ili kuvutia mizigo mingi zaidi kwenye bandari.
Mwenyekiti wa Chama cha Ukusanyaji na Utawanyaji wa Shehena Hawa Mohamed amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa katika kuwakumbusha kanuni ili kwenda kutekeleza maeneo yao.
Hawa amesema kuwa ombi lao kwa TASAC ni kupunguza gharama ili kuweza kuwa katika usawa wa kufanya biashara hiyo.
Mdau kutoka Kampuni ya Cuactus Eliud Haonga amesema kuwa TASAC imekuwa karibu kwao kwenye kuwahudumia katika kurahisisha kufanya kazi zao.
Amesema kuwa mkutano huo unakwenda kuboresha mazingira ya kufanya kazi ni pamoja kuzielewa kanuni na sheria.