Naibu Katibu Mkuu, Utawala Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khalid Masoud amewataka Waandishi wa Habari Vijana kuandika na kuziwasilisha kwa weledi habari zinazozingatia maslah ya Umma ili kuepuka migogoro katika jamii.
Wito huo ameutoa leo kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mohammed Mussa katika hafla ya ugawaji wa tunzo kwa wanaandishi wa habari chipukizi wa kijamii na ubunifu, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Skuli ya komputa na Mawasiliano ya Umma Kilimani Mkoa ya Mjini Magharib Unguja ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari.
Amesema ni vyema kuandika habari kwa kuzingaia kanuni, taratibu na Msingi ya Uandishi wa habari ili kuleta tija kwa jamii.
“Siku hizi kila mmoja ni mwandishi wa habari hivyo wito wangu kwenu nyinyi waandishi chipukizi kuandika habari kwa weledi hasa habari zinazozingata maslah ya Umma,” amesema.
Aidha amesema kuwa, Serikali ya awamu ya nane kupitia Wizara ya Habari inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha waandishi wa habari nchini wanafanyakazi bila ya vikwazo ili kuona watekeleza majukumu yao na kuwapatia taarifa wananchi kwa usahihi.
Hata hivyo akizungumzia siku ya uhuru wa vyombo vya habar amesema kuwa, siku hiyo ni muhumu ambayo inatoa fursa ya kuthamini michango inayotolewa katika kukuza tasnia ya habari pamoja na kuyatathmini mazuri ili kuyaendeleza na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikumba tasni hiyo kwa maslahi ya wanatasnia na jamii.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Skuli ya Komputa na Mawasiliano ya Umma Hamza chande amesema kuwa, Serikali itaendelea kuimarisha Skuli ya habari ili kuendelea kuwaandaa vyema wanahabari mahiri na kukuza tasnia ya habari.
“Tutaendelea kuwaandaa wanahabari mahiri kwa kuanda mashindano yaliyolenga kuibua na kuendeleza vipaji vyao katika tasnia ya habari,” amesema.
Mapema Mkurugezi Idara ya habari Maelezo Salum Ramadhan amesema kuwa, Wizara itaendelea kushirikiana na chuo cha habari katika kuzalisha watendaji wenye sifa.
“Wizara imeona juhudi hizo zinakwenda kuleta matoke chanya katika sekta ya habari na kuweza kuzalisha watendaji wenye sifa katika tasnia ya habari,” amesema.
Hata hivyo amesema, Wizara inaendelea kuwashajihisha wadau wa habari ikiwemo TAMWA, ZBC, MCT na wengene kuanzisha mashindano kama hayo ambayo yanalea waandishi wa habari na kuleta matoke chanya kwa waandishi wa habari.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na yanahusisha Wanafunzi na Waandishi wa habari chipukizi.